FAQs

 

Majibu ya Maulizo

Naweza kununua bidhaa kupitia website/tovuti hii?

Ndio! Bofya SHOP ili uweze kununua bidhaa yoyote kwenye website/tovuti hii na ukaletewa bidhaa mahali popote ulipo. Kumbuka, gharama za usafiri ni juu ya mteja.

Naweza kulipia baada ya kupokea bidhaa?

Ndio! Unaweza kulipia baada ya kupokea bidhaa yako na kujiridhisha usahihi wa bidhaa na kiwango au idadi.

Naweza kuwa wakala?

Ndio! Unaweza kuwa wakala wa bidhaa zetu mahali popote ulipo. Utauziwa bidhaa kwa bei ya jumla nawe utauza kwa bei ya rejareja elekezi

 

Majibu ya Maulizo

Naweza kurudisha bidhaa?

Hapana! Baada ya kununua bidhaa hautaruhusiwa kurudisha bidhaa hiyo, hivyo mteja unashauriwa kuhakiki bidhaa yako kabla hujaweka oda.

Delivery ni BURE?

Hapana! Utalipia delivery kutokana na umbali na mahali ulipo.

Mna branch mikoani?

Ndio! Makao makuu yetu yapo Dar es Salaam, lakini tuna mawakala, Tanga, Arusha, Mwanza, Dodoma, Kilimanjaro na Manyara.

 

Majibu ya Maulizo

Unga wenu wa Tamu Lishe unaweza tumiwa na mtoto wa kuanzia umri gani?

Unga wa Tamu Lishe unaweza tumiwa na mtoto wa kuanzia umri wa miezi 6 mpaka watu wazima, lakini pia unga huu unaweza tumiwa na wazee na hata mama wajawazito.

Kuna utofauti gani wa Tamu Lishe na Unga mwingine wowote wa lishe uliopo sokoni?

Unga wa Tamu Lishe unamchanganyiko wa kipekee na tofauti ukilinganisha na unga mwingine wote wa lishe ulipo sokoni, bei zetu ni nafuu na tumezingatia uwiano wa nafaka ili kukupatia ubora unaostahili.

Kwa mikoa ambayo hamna mawakala mnatuma bidhaa?

Ndio! Unaweza tumiwa bidhaa mahali popote ulipo, ila tu utagharamikia gharama zote za usafiri.